Vyombo vya habari vyaibua upya kwamba kifo cha Princess Diana Hakikusababishwa na Ajali

princess dianaUtata kuhusu kifo cha Diana na mpenzi wake Dodi al Fayed, baada ya mamlaka ya habari uingereza kutoa taarifa kwamba Diana na Fayed waliuawa na kikosi maalumu cha jeshi la uingereza.

Ingawa dola million 7 za kimarekani za Polisi wa Ufaransa na uingereza zilitumika kufanya uchunguzi wa vifo hivyo na kutoa ripoti yao ya kwamba kifo cha Diana, Al fayed na dereva wao Henri Paul’s mwaka 1997 kilisababishwa na ajali kuficha mauaji hayo.

Kesi ambayo imekuwa ikiendeshwa , sgt Danny Nightingale ambaye amepatikana na kosa la kumiliki silaha bila kibali maalumu. Baadhi ya vidhibiti ilikuwa na barua kutoka kwa mwanajeshi wa zamani akituhumu kwamba “kikosi maalumu cha kijeshi kilitumika kufanya mauaji ya Pricess Diana”, linalipoti gazeti moja.

Siku ya Jumamosi mamlaka ya Scotland ilisema kwamba askali ya kiingereza wamekuwa wakiangalia habari mpya zinazohusisha kifa cha Diana na Al Fayed lakini askari hao walikataa kutoa habari kuhusu taarifa hizo.

Msemaji mmoja wa Scotland anasema “Mamlaka ya kipolisi imekuwa ikizifuatilia habari walizozipokea zinazohusiana na kifo cha Diana na Mpenzi wake kujaribu kujua kama zinaukweli ndani yake”. aliendelea akisema ” Uchunguzi utafanywa na mtaalamu wa makosa ya jinai ikihusisha kikosi maalum”

 

Lakini aliendelea kwa kusema kwamba ” huu sio uchunguzi mpya na wala hautokani na kikosi cha uchunguzi wa matukio hayo cha mwaka 1997″

Baba mzazi wa Dodi al fayed mzee Mohammad al Fayed hakuwa na usemi wowote kuhusu jambo hilo lakini anataarifa kuhusu uchunguzi huo unaofanywa na polisi,  ila msemaji wa mzee Mohammad anasema ” Mzee huyo anatarajia ya kwamba uchunguzi ukamilike na aweze kujua matokeo yake”.

Mzee huyo amekuwa akiamini kwamba mwanae na Diana waliuawa na wamekuwa wahanga wa kufunika jambo fulani lakini kesi zote alizozifungua alishindwa kwa kukosa ushahidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s