Mtu Mzee kuliko wote Duniani Apatikana huko Bolivia akiwa na Miaka 123

bolivia2Kutoka kijiji cha FRASQUIA, huko Bolivia  — Kama nyaraka za serikali ya bolivia hazina makosa Camero Flores Laura ndio mtu mzee kuliko wote duniani ambaye nyaraka zake za kuzaliwa zimetunzwa.

Wezi uliopita alifikisha miaka 123. Mzee huyu anaishi kwenye nyumba ya nyasi ambayo haijasakafiwa ndani ikiwa imejitenga karibu na ziwa TITIcaca. Mzee huyu hajasoma, azungumzi kihispania wala hana meno.

Camelo anatembea bila mkongojo na wala havai miwani. Anazungumza lugha ya Aymara na sauti ya upole, iliakusikie inabidi umsogeleee kwa ukaribu sikioni kwake.

“Macho yango yanaona giza kwa mbali, lakini nilikua naona vizuri. Nimewaona mkija,” Anawaambia waandishi wa habari waliomtembelea kutuka kituo kimoja cha Televisheni hapo Bolivia.

Akipita kwenye njia ya vumbi, Camala anawasalimia huku akiwapa mkono na tabasamu nzuri na akakaa kwenye mwamba tayari kwa maongezi.

Kulingana na rekodi za (Guinness World Records)  kumbukumbu zinasema kwamba mtu aliyepata kuishi kwa muda mrefu na kumbukumbu zake kuwepo ambazo zilithibitishwa alikuwasays  Misao Okawa, mwanamke wa kijapani aliyekuwa na umri wa miaka 115 , wakati huo huo kunarekodi nyingine za miaka 122 na siku 164 : Jeanne Calment wa ufaransa ambaye alifariki mwaka 1997.

Mjukuu wake mwenye umri wa miaka 27, Edwin anasema ya kwamba hakujua kitu kinachoitwa Guinness na pia msemaji wa kundi kuhusu mzee huyo.

“Ninaweza kuwa na miaka 100 na zaidi ” anasema Flores.

Mkurugenzi wa usajiri wa Bolivia , Eugenio Condori alionyesha nyaraka zinazohusisha siku ya kuzaliwa kwa mzee Carmelo Flores kuwa ni tarehe 16-7-1890.

Mkurugenzi huyo anasema ya kwamba wakati huo hakukuwa na vyeti vya kuzaliwa mpaka mwaka 1940. Wakati huo umri wa mtu ulirekodiwa wakati wa ubatizo kwa kupata cheti cha ubatizo kutoka kanisa la katoliki lililopo hapo karibu kwa ushahiddi wa watu wawili wakati wa ubatizo.

”Kwa nchi yetu cheti cha ubatizo kinatambulika kwasababu siku hizo mapadri ndio waliotoa vyeti hivyo na walikuwa wamesoma” anasema Eugenio Condori. Anasema hakuwaonyesha cheti hicho watu wa shirika la utangazaji AP kwa sababu  ni nyaraka ya mtu binafsi.

Mjukuu wake anasema kwamba familia yake ilionyesha cheti chake cha ubatizo ili aweze kupata malipo ya kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya uzeeni.

bolivia1

Je ni kwanini basi Flores ameweza kuishi muda mrefu?

Flores anasema “Huwa ninatembea sana, hilo ndio jambo pekee. Hutoka kwenda malishoni kuchunga mifugo” amekuwa akimiliki ngombe na kondoo. ” anasema huwa hali tambi au wali yeye hula mtama tu. Alikuwa mkulima wa viazi na maharagwe.

Flores yeye hunywa maji ya mto yanayotokea kwenye mteremko wa mlima illampu, moja ya  milima mirefu huko Bolivia.

Mzee huyu yeye hatumii pombe lakini akiwa kijana alishawahi kutumia, na anapenda sana kitimoto (nyama ya Nguruwe)  ingawa ni adimu huko. Vile vile anakumbuka akiwinda na kula fisi akiwa kijana, hajawahi kwenda mbali zaidi ya mji wa LA Paz kilometa 80 kutoka hapo anapoishi na hajawahi kuumwa sana.

Anamkumbuka sana mkewe aliyefariki zaidi ya miaka kumi iliyopita.

bolivia3

Maishani mwake alipata watoto watatu ingawa ni mmoja tu aliye hai mwenye miaka 67, wajukuu 40 na watoto wa wajukuu zake 17 ingawa wengi wao waliondoka Frasquia na wanaishi mwendo wa masaa mawili karibu na barabara ya kwenda Warisata.

Edwins Flores, anayeishi karibu naye akiwa na mke na watoto wawili, anasema babu yake alifanya kazi kwa mkulima mmoja mkubwa aliyekuwa akimiliki kijiji cha Frasquia mpaka 1952 lakini eneo hilo likabinafsishwa.

bolivia6 bolivia5 bolivia4

kutoka kwa mwandishi  Frank Bajak kutoka  Lima, Peru.

Habari imetafsiriwa na Awali Ambonisye Mwaisanila.

Advertisements