Turinge ujio wa Obama Tanzania

Turinge ujio wa Obama Tanzania LEO Rais Barack Obama anayeongoza taifa kubwa na lenye nguvu duniani, Marekani, atakanyaga ardhi ya Tanzania na bila shaka ataleta ‘baraka’ tele nchini kama asili ya jina lake lilivyo. Ujio wa Obama nchini mwetu kwa hakika ni baraka, na kama Waswahili wanavyosema, mgeni njoo, wenyeji tupone. Ni faida za kiuchumi, kijamii na kisiasa kama tutakavyoangalia, japo kidogo katika makala haya.

Ilikuwa hayawi hayawi, hatimaye yamekuwa kwani hapo katikati baadhi ya vyombo vya habari vilifikia kuandika kwamba Obama amesitisha ziara yake hapa Tanzania na vingine vikawa vinaibua vitu ambavyo hata havijai kwenye kiganja cha mkono kama sababu ambayo eti ilitaka imfanye Obama asije Tanzania. Kwa mfano, kuna hawa waliodai kwamba yupo ofisa mmoja wa Tanzania aliyemnyanyasa mmoja wa ‘wanafamilia’ wake wakati akiishi huko Marekani na kwa hiyo Obama alitakiwa asije kwa hilo tu… hilo tu . Kuna waliokuwa wanahoji sana kwa nini aje Tanzania na si Kenya kuliko asili yake kwa upande wa baba yake. Yaani kwa vile Tanzania inapakana na Kenya inakuwa nongwa, kana kwamba hii itakuwa safari yake ya kwanza na ya mwisho kuja Afrika akiwa Rais ama kama vile ni Rais wa kibaguzi.Hawahoji Senegal alikoanzia wala Afrika Kusini ila Tanzania! Chaguo la Watanzania Waseme watakavyo lakini sisi Watanzania tunakukaribisha ndugu yetu Obama kwa mikono miwili. Tunakupenda siku zote na kukuombea toka ulipoanza harakati za kugombea urais wa Marekani. Yaani ni kama vile ulituona mwaka ule ulipokuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kutawala nchi yako. Siku uliotangazwa kumshinda mgombea wa Republican, John Mc- Cain, kwa kweli karibu kila Mtanzania alifurahi na kushangilia. Wapo waliokaa usiku kucha kufuatilia matokeo hadi hotuba ulioitoa baada ya ushindi wako wa kihistoria usiku wa manane (kwa sasa za Tanzania). Furaha waliokuwa nayo Watanzania ni kama walijua kuna siku moja utawatembelea wewe mwenyewe, kuwajulia hali na kusaidiana nao katika kuboresha hali zao za misha na za watu wote wa dunia. Karibu Tanzania. Watanzania walikuwa pia na mioyo ya furaha na bashasha siku ya Januari 20 mwaka, 2009, siku ambayo uliapishwa kuongoza Marekani. Watanzania kwa umoja wao walifurahi sana. Watanzania pia walikuwa na furaha ile ile pale miezi tisa tu baada ya kuingia Ikulu ya Marekani ulipoteuliwa kuwa Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobeli.

Ulipochaguliwa tena kuongoza Wamarekani wenzako kwa mara ya pili katika uchaguzi wa Novemba mwaka jana dhidi ya
mgombea wa Republican, Mitt Romney, Watanzania, kama ilivyokuwa mwaka 2009, walikuwa nyuma yako, wakakushangilia,
kukushabikia na kukuombea baraka. Tunatarajia katika ziara yako utatuambia mazuri ya kutusaidia katika uongozi wa nchi yetu kama ulivyowaambia Ghana katika safari yako ya masaa 36 nchini humo mwaka 2009. Ulisema “Afrika haihitaji kutegemea nguvu ya kiongozi bali inahitaji kujenga taasisi imara na zenye nguvu.” Nasi tunaandaa Katiba mpya inayoimarisha taasisi zetu na bila shaka utatupa maneno ya busara. Watanzania turinge Ujio wa Obama, ikiwa ni takribani miezi mitatu toka tutembelewe na kiongozi mwingine wa taifa kubwa duniani la China, Xi Jinping, ni jambo la kujivunia na linawafanya baadhi ya watu kutuonea wivu, lakini kama walivyowahi kuimba wanamuziki wa Vijana Jazz Band, ‘kasoro ya binadamu toka enzi na enzi ni kutopenda maendeleo ya mwingine’.
Sisi tusijali maneno kwani Waswahili wanasema pia kwamba “kelele za chura hazimzuii ng’ombe kunywa maji.” Xi Jiping alikuja
nchini Machi 28, ambapo Tanzania ilikuwa nchi yake ya kwanza kutembelea Afrika baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo
kubwa Machi 14. Lazima turinge.

via Turinge ujio wa Obama Tanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s