Obama anakuja tutegemee nini?

obama1_on phone
Marekani, taifa linaloongoza duniani kwa nguvu kiuchumi na kijeshi liliingia rasmi katika uhusiano wa kibalozi na Tanganyika mwaka 1961. Uhusiano huu umeenedelea hata sasa baada ya nchi mbili huru -Tanganyika na Zanzibar kuungana Aprili 26, mwaka 1964 kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Balozi wa mwanzo wa Marekani hapa nchini ni William R. Duggan ambaye alipandishwa hadhi kuwa Balozi kamili baada ya Tanganyika kupata uhuru Desemba mwka 1961. Uhusiano wa Tanzania na Marekani una manufaa kwa pande zote mbili kwa sababu Tanzania imo katika bara la Afrika ambalo limejaaliwa kuwana raslinmali za aina na aina. Kutokana na utajiri huo Afrika sasa ndio kimbilio la Mataifa makubwa ya Ulaya na Marekani na Asia, kwa mahitaji ya raslimali ya Mafuta na Gesi Asilia ambazo ndizo zinazotawala katika akili za watu wa Mataifa makubwa. Mazingira hayo yameibua msamiati katika mataifa hayo kwamba:’Oil and Natural Gas is new scramble for Africa’ ukiwa na maana: ‘Afrika kimbilio la Mataifa makubwa kwa Mafuta na Gesi Asilia.’ Tanzania imejaaliwa kuwa na rasilimali ya Gesi Asilia, pia kuna fununu za kuwepo kwa mafuta na hata uranium.Ukiacha rasilimali hizo, bado Tanzania inautitiri wa rasilimali za baharini, mbuga za wanyama, madini ya aina kwa aina, yote hii ni neema kubwa kwa wananci wa Tanzania. Hata hivyo, swali linaloulizwa ni kwa kiasi gani rasilimali hizo zinavyoweza kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Mataifa makubwa? – yakiongozwana Marekani. Je kukua na kushamiri kwa uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kisiasa ni sababu mojawapo ya rasilimali au sera yetu ya mambo ya nje; ndiyo inayowafanya wakubwa wa dunia kumiminika kuja Tanzania? Ni suala lililowazi kuwa Mataifa ya Afrika hivi sasa yanakabiliwa na changamoto ya kinyang’anyiro kipya cha Mataifa makubwa ya Ulaya yenye nguvu za kiuchumi pamoja na Marekani ambapo umuhimu wa mafuta na gesi asilia  katika bara la Afrika, na nguvu ya kisiasa na kiuchumi; ni sehemu ya sababu ambazo mataifa makubwa yanatupia jicho Bara hili. Kuthibitisha hilo, mapema julai mwaka huu, Rais wa Marekani, Barack Obama atafanya ziara rasmi ya Kiserikali.Hii ni ziara ya pili ya Rais Barack Hussein Obama katika Bara la Afrika. Mwezi Julai mwaka 2009, Obama alifanya ziara nchini Ghana. Kwenye uwanja wa diplomasia, ziara ya Rais Obama itakayoanzia Dar es Salaam Tanzania ni mafanikio ya sera ya Tanzania ya mambo ya nje, ni kielelezo cha namna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyokubalika na kuthaminiwa  katika medani za kimataifa. Na iwe itakavyokuwa, suala ambalo linaulizwa na wengi ni; je, kwanini kiongozi huyo wa Taifa kubwa anatembelea Tanzania? Kwanza Tanzania ni nchi salama, inapewa sfa ya kuwa kinara wa amani amani na utulivu, pili; Tanzania ina rasilimali nyingi, hivyo ni jambo la wazi kuwa Mataifa makubwa kama Marekani yangependa kuwekeza katika nchi kama hii. Marekani ni nchi yenye viwanda vingi, viwanda vinahitaji mali ghafi, lakini pia bidhaa zinazozalishwa viwandani nchini humo zinahitaji soko, na kwa maana hiyo taifa hilo haliwezi kupuuzia soko la Tanzania ambayo watu milioni 44.9, ukiwekeza Tanzania umewekeza Afrika Mashariki, umewekeza ukanda wa Maziwa Makuu. Ujio wa Obama unaweza kusema kuwa ni kinyanga’nyiro kipya baina na  kama mbio za kupokezana vijiti baina ya Marekani na China (New Scramble or a US–Chinese race for Africa). Tayari Rais wa China, Xi Jinping alifanya ziara rasmi ya Kiserikali mapema mwaka huu. Obama anakuwa Rais wa tatu wa Marekani kutembelea Tanzania, Bill Clinton alikuja mwaka 1998 wakati mtangulizi wa Obama, Rais George Bush alifanya ziara mwaka 2008. Taarifa ya Ubalozi wa Marekani kuhusu ziara ya Rais Obama, inaonyesha kwamba Rais Obama atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali, ikiwamo ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika. Nchi yenye amani na utulivu kama Tanzania, inaweza kusonga mbele kiuchumi kwa kutumia fursa ya uwekezaji unaowekezwa moja kwa moja kutoka nje ( Foreign Direct Investment-FDI) ni sehemu mojawapo ya njia ya kukuza uchumi ambapo  uwekezaji wa makampuni ya nje  ni muhimu katika uchumi wa kileo chini ya biashara huru na utandawazi. Uwekezaji huo unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mwanachama wa Shirika la Kimataifa la Biashara(WTO) ambapo kwenye WTO nchi wanachama zinafungika katika kuheshimu makubaliano ya kibisahara. Siku hizi wataalam katika Tasnia ya uhusiano wa kimataifa wanasema, nguvu za soko huria, mashirika makubwa kama Shirika la Biashara la Kimataifa (WTO), Shirika la Fedha Duniani (IMF) na enki ya Dunia (WB) zinaelekea kuwa sawa na Dola kamili (Sovereign State). Faida kubwa ambayo kukiwa na FDI katika nchi ni kuwepo kwa fursa za ajira, mapato kuongezeka na wawekezaji kulipa kodi Serikalini na hivyo kuongeza katika mapato ya Serikali na kukuza uchumi. Faida nyengine ya FDI ni kubadilishana teknolojia, utalaam na pia kuongezeka kwa fedha za kigeni katika nchi. Ninategemea ujio wa Rais Obama utalate neema katika uwekezaji wa FDI hapa Tanzania. Mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini yanawavuta wawekezaji wakubwa na makini kama Marekani kufikiria kuwekeza katika nchi yetu. “Marekani inafurahia sana uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania, hakuna nchi nyengine yeyote katika Afrika ambako Marekani inawekeza muda wake, rasilimali zake kuliko Tanzania kwa sasa kwa sababu Tanzania ni nchi nzuri kufanyanayo biashara na ushirikiano wa kiuchumi.” Hayo ni matamshi yaliyotolewa na Mwanadiplomasia wa Marekani, Balozi Ron Kirk alipozungumza na Rais Jakaya Kikwete hapa nchini. Kwa hakika matamshi haya yanathibitisha namna uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi ulivyotamalaki baina ya Marekani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivi leo Marekani ina shauku kubwa ya kutawala soko la bidhaa Afrika, huku Afrika likibaki kuwa Bara pekee lenye akiba nyingi ya rasilimali na kwa msingi huo ndio maana kuna taasisi za Marekani  kama vile United States Africa Command (AFRICOM) na United States Africa Army (USARAF).

Inaelezwa kuwa taasisi hizo za Marekani zilizopo Afrika, shabaha yake kuu ni kusimamia maslahi ya Marekani katika Afrika na  kusisimua na kuhamasisha mabadiliko mujarab  katika bara la Afrika kwa kuzima vikundi vyenye misimamo hatarishi huku shabaha nyingine ikiwa ni kutengeneza mazingira salama kwa biashara na ukuaji wa demokrasia. Mbali na suala la kiuchumi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wote iko mstari wa mbele kuhimiza amani na utulivu, kuanzia kwenye Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kote huko Tanzania ni kinara wa kuhimiza, kuhamasisha umoja na mshikamano pamoja na utulivu. Wakati huu, askari wa Tanzania wako Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakitekeleza mpango wa Umoja wa Mataifa na ule wa Umoja wa Afrika kurejesha amani na utulivu nchini humo. Bila shaka kwa mataifa makubwa, hasa Marekani inapenda kuziunga mkono nchi kama Tanzania katika kutunza amani. Ziara ya Obama itawatia nguvu na shime askari wa Tanzania na wale wa Afrika Kusini walioko DRC, nadhani ziara hii italeta mwanga mpya wa ukuzaji wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya nchi mbili hizi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s