MAMBO 7 AMBAYO MARA CHACHE SANA UTAAMBIWA AU KUYASIKIA KUHUSU MAHUSIANO/NDOA

foretag Zipo nyakati unaweza kujikuta unaenda kitandani ukiwa na hasira, na yamkini ukaamka asubuhi ukiwa na hasira zaidi ya ulizo lala nazo.
Tofauti baina ya jinsia hizi mbili kama nilivyogusia kwenye jambo la pili ziko katika maeneo mbali mbali ya mahusiano yetu na mojawapo ni tofauti tulizonazo baina ya wanawake na wanaume hususani katika kuishuhulikia migogoro inayoibuka ndani ya mahusiano yetu. Yawezekana wewe ni mmoja wa wale wasio na hasira sana, muelewa, mwepesi wa kusamehe na kuchukuliana na hali, mara kwa mara unatamani mliongee jambo lililoleta utata baina yenu kabla halijakuwa kubwa na kuleta madhara. Tabia hii ni nzuri sana, lakini kwa bahati mbaya unakutana na mwenzako ambaye hakufunzwa vyema namna na jinsi ya kuishuhulikia migogoro. Unajua katika makuzi yetu wako ambao wamekuwa katika mazingira ambayo hayakuwaandaa kabisa kuja kuhusiana na bina damu mwingine yeyote, tabia zao wanazijua na kuziweza wao peke yao, ni ngumu hata kukaa na mtu huyu kwa lisaa limoja chini ya dari moja, katika saikolojia tunawaita “difficult personalities”. Unakuwa na mtu kama huyu kazini, kwa jinsi unavyoona tabia zake katika kuhusiana na wengine unajiuliza hivi mpenzi wake anaziweza vipi tabia zake? Sasa aina hii ya mtu unajikuta kwa bahati mbaya au nzuri labda ndio umehusiana naye katika mapenzi, kilasiku unategemea kuona mabadiliko lakini ndo maudhi yanazidi. Hata pale anapokuahidi kujitahidi kubadilika ili kukuridhisha bado unaona kama anaongeza machungu moyoni mwako. Kila siku unaona ‘bora hasira ulizokuwa nazo jana’. Ili kuepuka hali hii, kuwa macho sana wakati wa mahusiano, viko vitu vingi sana vya kuangalia katika tabia za mtu kabla hujaamua kuanza naye mahusiano ya kimapenzi. Hii habari yakujipa moyo na matumaini yasiyo rasmi eti ‘atabadilika tu!!’ ‘nitajitahidi kumrekebisha’…. ‘Mungu atambadilisha’ . Wengine wameshindikana tangia kwao tokea utoto we umekutana naye juzi tu utamuwezea wapi kama sio kujinunulia kitanzi kwa hela yako mwenyewe? Wako wengi waliotarajia hivyo hivyo kuwa wapenzi wao watabadilika sikumoja, bahati mbaya walipoamua kurasimisha mahusiano yao na wengine kuingia kwenye ndoa tabia ndo zikazidi kuwa mbovu na za kukatisha tamaa. “usijaribu kina cha maji kwa kuingiza mguu” Watch out.

By Chris Mauki
http://www.facebook.com/chris.mauki

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s